Katika
mapori na hifadhi za hapa nchini na kwengineko Africa, ndege ajulikanae kama
fundi chuma hupatikani. Ndege huyu ni maarufu kwa kujenga viota vikubwa na
imara sana. Ujenzi hufanywa na dume kwa lengo la kumrubuni jike ili aungane nae
kuanzisha familia kama ilivyo ada kwa ndege wengi.
Fundi
chuma hujenga viota vikubwa na kwa kutumia malighafi mbalimbali ambazo anaweza
kuzipata ktk maeneo anayopita. hutumia udongo, miti, mawe madogo madogo na
wakati mwingine hata vipande vya mifuko ya plastiki na nylon vimewahi kutwa ktk
kiota cha fundi chuma. Ilihali ndege wengine hutumia miti na majani
kutengenezea viota vyao.
Jambo
moja ambalo lilipita masikioni mwangu ni kwamba, cheza mbali na kiota cha fundi
chuma. Inaelezwa ya kwamba (sina ushahidi) ukikiharibu au kubomoa kiota cha
fundi chuma (ndege), basi kama ulikuwa una nyumba yako, hiyo nyumba yako ipo
hatarani kupotea kwa namna yoyote ile - mafuriko au moto. wapashaji habari
walienda mbele na kusema kuwa endapo kama hauna nyumba, basi nafasi ya wewe
kuja kuwa na nyumba yako ndio inakuwa imetoweka.
Nilidokezwa
ya kwamba hii dhana ipo miongoni mwa makabila mengi ya hapa nchini. Ukweli ni
kwamba hii issue ni kama sumu, haionjwi! so ukweli wake inabidi uupate kwa
kupitia neno la mdomoni. Mara nyingi fundi chuma huwa na tabia ya kukikacha
kiota chake endapo atagundua kuwa hakivutii majike.
picha
juu ni kiota cha fundi chuma (hilo fungu unaloliona ktk huo mti) kilichojengwa
ktk mti pembezoni mwa Mto Ruaha, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.