Simba ashangaza
dunia baada ya kukutwa akimnyonyesha mtoto wa chui huko katika hifadhi ya
taifa ya wanyama pori ya Ngorongoro nchini Tanzania
Kitendo
hicho kisicho cha kawaida kilishuhudiwa na Joop Van Der Linde mgeni
aliyetembelea eneo la Ndutu safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la
uhifadhi la wanyma pori la Ngorongoro. Limekuwa tukio la ajabu kwa sababu ya
utofauti wa jamii ya wanyama hawa, Simba akitokea jamii ya Leo na Chui akitokea
jamii ya Tigris. Wote wakiwa ni Panthera.
Ndipo
alipo muona Simba huyo mwenye umri wa miaka mitano aliyepewa jina la
Nosikitok mwenye watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28.
Sio kitu ambacho nilijuwa ambapo simba angeweza kuwalea watoto wa simba
mwengine, hiki ni kisa tofauti sana.
Sina kisa chengine chochote nikijuacho kati ya familia ya mnyama paka
kwa mfano pale ambapo mnyama mmoja amechukua mwana wa mnyama mwengine katika
familia hiyo hiyo na kumnyonyesha.
Simba wengi wa kike huwauwa watoto wa chui wanapokutana nao, na huwaona
kama wapinzani katika mapambano ya kutafuta chakula.
Daktari Hunter anasema Nosikitok ana watoto wachanga walio na umri sawa
na mwana huyo wa chui wakiwa na wiki mbili hadi tatu hivi.