SERENGETI, Mara:23.07.2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, jana aliwapokea Mabilionea 26 katika Mbuga ya Serengeti.
Mabilionea hao walifuatana na wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.
Wageni hao ambao wanatoka katika club ya mabilionea ya YPO (Young Presidents Organisation) wanatoka mabara yote duniani.
Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa vivutio vya utalii barani Afrika na duniani.
Katika ziara hiyo ya nchi nane (8) ambazo ni: Uingereza, Rwanda, Tanzania, Maldeves, Nepal, Bhutan, Rajastan na nchi moja nyingine, wageni hao wamemwaga sifa kem kem kwa vivutio vya Tanzania.
Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Prof. Maghembe aliwakaribisha nchini Tanzania na kuwaambia kuwa maajabu ya Dunia yamebebwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
"Hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivorous) na wale wanaokula nyama (carnivorous) kama ilivyo katika mbuga hiyo ya Serengeti.
Aidha, Prof. Maghembe aliwaeleza wageni wake kuwa uhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia.
Aliwaomba wageni hao wawe Mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo pekee la amani lenye vivutio vyenye ubora wa pekee duniani.
Alisema hatua hiyo italeta watalii wengi nakuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokuwa kwa wastsni wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.
 
Top