Watanzania
wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kutembelea hifadhi za Taifa (TANAPA)
ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kuhamasisha watanzania kuweza kutembelea
hifadhi za taifa yenye kaulimbiu isemayo tembelea hifadhi za taifa ufaidike.
Baadhi
ya Wanyama wanaopatika katika mbuga zilizochini ya Hifadhi ya Taifa TANAPA
Hayo
yamesemwa na Victor Raphael Kintansi ambaye ni kaimu meneja masoko wa hifadhi
ya taifa (TANAPA)wakati akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa utalii
katika press conference iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach
Resort iliyopo eneo la Sahare jijini Tanga.
Bw,
Victor amesema lengo la kampeni hiyo ni kupata watalii wa ndani wapatao laki
tano kwa mwaka huu kama ongezeko la watalii wa ndani tofauti na miaka mingine
iliyopita.
Aidha
ameongeza kuwa zipo zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa watanzania wanaotembelea
hifadhi mbalimbali za taifa mara baada ya watalii hao kutembelea hifadhi yoyote
kwa zaidi ya mara moja.
Sambamba
na hayo ameeleza kuwa mtalii wa ndani atakayeweza kutembelea hifadhi yoyote
zaidi ya mara nne kipindi hiki cha kampeni atapata zawadi ya juu kutoka shirika
la hifadhi za Taifa TANAPA ya kumpeleka mtanzania katika hifadhi ya taifa ya
Serengeti au Gombe na kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano kwa
gharama za TANAPA.
Kwa upande wake Pellagy R. Marandu ambaye ni Afisa Utalii
mwandamizi kutoka hifadhi ya taifa ya Mkomazi amesema watanzania wengi
wameonekana kuwa bado hawajaelewa umuhimu wa kutembelea vivutio vingi
kwakuhofia kuwa gharama ni kubwa huku akiwatoa hofu watanzania kuwa gharama zao
zinatofautioana na watalii wa nje.