Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema
inakusudia kuimarisha sekta ya utalii kwa kuweka mawakala wao katika
nchi za nje ili kufanyakazi ya
kuitangaza Zanzibar katika nchi mbalimbali ili
kuwavuta watalii kujanchini.
Akizungumza na Mwandishi wetu
Afisa Masoko na utangazaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Halfani Ali
Mohammed
amesema ili kuukuza utalii Zanzibar
lazima serikali itekeleze azma yake ya kuweka
wakala katika nchi mbalimbali duniani kutangaza vivutio vya utalii
viliopo nchini.
Hata hivyo
amesema mbali na kuwepo kwa kituo cha cha wakala
katika nchi ya India kinachotangaza utalii wa
Zanzibar lakini pia serikali
imekusudia kufungua vituo vyengine vipya katika
nchi ya China, Israel na Urusi ili kuendelea kutangaza utalii wa
Zanzibar.
Aidha amesema katika hatua hizo
zinazotarajiwa kuchukuliwa ametoa wito kwa wakaazi wa
zanziabr kutunza na kuhifadhi maeneo ya
vivutio vya utalii vilivyopo nchini pamoja
na kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Zaidi ya watalii Laki tatu
sabini na sita Elfu mia mbili arobaini na mbili
walitembelea Zanzibar kwa mwaka 2016 huku wageni kutoka nchi za
Ujerumani, Italy, Marekani na Israel wanaongoza kuitembelea Zanzibar.