Tanzania
licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii, lakini pia inajivunia kuwa na faru
mweusi jike ambae ndie faru mzee zaidi duniani.
Faru
huyo maarufu kwa jina la Fausta hivi sasa amehifadhiwa katika eneo maalumu
baada ya afya yake kudhoofika. Aboubakar Famau hivi karibuni alikuwa
katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na kutuandalia taarifa ifuatayo.
FARU
Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani, mwaka
huu amefikisha umri wa miaka 54.
Faru
Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, lakini kutokana na uzee
wake huo, sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona vizuri.
Kufuatia
hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya
hifadhi hiyo.
Hatua
ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia
kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani Fisi na Simba.