Picha hiyo iliopigwa na mpiga picha wa
Afrika Kusini Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi katika mbuga ya
wanyama pori ya Hluhluwe Imfolozi iko umbali wa kilometa 280 kaskazini mwa mji
wa Durban Afrika Kusini.
Wawindaji haramu walimuua mnyama huyo
usiku kabla ya kumtoa pembe zake.
Stirton alipiga picha hiyo ikiwa
miongoni mwa uchunguzi kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru.
Mpiga picha huyo alizuru zaidi ya maeneo
30 uliofanyika uhalifu huo wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa
kuogofya.
Mwanangu wa kwanza atazaliwa mnamo mwezi
Februari ; nina umri wa miaka 48. Unaweza kupoteza utu mara nyengine.
Stirton, ambaye alipokea tuzo hiyo
katika tamasha la chakula cha jioni lililofanyika katika jumba la kumbukumbu
mjini London , anaamini kwamba unyama huo aliofanyiwa faru huyo ulitekelezwa na
wakaazi wa eneo hilo.
Lengo kubwa la uwindaji huo ni kuuza
pembe mbili za faru huyo kwa wafanyibiashara.
Wafanyibiashara hao baadaye huzipeleka
pembe hizo hadi Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama hata Vietnam.
Katika mataifa hayo ya bara Asia, pembe
za faru zina thamani ya juu ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya
Cocaine.
Biashara hiyo hupata msukumo wa imani
kwamba sawa na kucha za vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote
kutoka saratani hadi mawe ya figo.
''Swala la kuangamia kwa baadhi ya
wanyama ni la kweli na faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea
kuangamia kwa kiwango kikubwa na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua
picha yangu kwa kuwa inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine''.
Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la
majaji hao wa WPY, alisema kuwa picha hiyo ya faru ilikuwa na athari kubwa
katika jopo lake.
''Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa
lakini ukweli ni kwamba picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana kwamba
unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa
sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani''.