Sieny ni eneo lililopo katika Kijiji cha Ngira, Wilayani Hai Mkoani
Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania, ni miongoni mwa maeneo yanayoheshimika
kutokana na imani ya kabila la Wachaga (wamachame) waishio katika eneo hilo.
Ni katika eneo hilo, ndio kunapatikana Daraja la Mungu ambalo wakazi
wake wanaamini limejengwa na Mungu, lakini pia kuna mapango yanayotumika kwa
matambiko.
Miaka ya nyuma ya 1979 eneo hili lilikuwa maarufu sana kwa wakazi wa
Kijiji cha Ngira na jirani (Sonu, Uswaa,
Mudio na Masama) walikuwa wanakwenda kuabudu na kufanya matambiko mbalimbali
wakiamini lolote linajibiwa na Mungu hata kuomba mvua na kupona magonjwa
mbalimbali.