Na
Dixon Busagaga, Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MPANDA
milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal raia wa Ureno
na wenzake wawili wameanza safari ya siku tano ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia
lango la Kilema ikiwa ni aina mpya ya utalii iliyoanza kushika kasi katika
hifadhi hiyo.
Hatua
hiyo inatokana na jitihada za shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kueendelea
kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,kwa kuanzisha aina mpya ya bidhaa
za utalii ili kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa
watalii.
Miongoni
mwa bidhaa hizo ni pamoja na zile zilizoanzishwa katika Hifadhi ya Taifa ya
Mlima Kilimajaro (KINAPA) ya kuzunguka mlima kwa kutumia Parachuti pamoja na kupanda
Mlima kwa kutumia Baiskeli, utalii ambao umeanza kushika kasi.
Juanito
Oiarzabal ambaye tayari ameweka rekodi nyingi duniani na kuingizwa katika
kitabu cha kumbukumbu kijulikanacho kama World Guinness Book amepanda mlima
Kilimanjaro na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia kwa kutumia
Baiskeli .
Mkurugenzi
wa Utali wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA ) Ibrahim Musa amesema
Oiarzabal atakuwa Mreno wa kwanza kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro
kwa kutumia baiskeli na kwamba aina hi ya utalii na rafiki kwa mazingira ya
Hifadhi.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Safari Bike Africa inayoratibu wa changamoto hii a kupanda Mlima
Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli,Mario Martos amesema hatua hii ni mwanzo wa
kufungua aina hii ya utali katika Hifadhi za Taifa za Arusha na Saadan.
Shirika
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
limeweka utaratibu wa kufanya vipimo kwa wapandaji wa Mlima kwa wanao tumia
Baiskeli pia kabla ya kuanza safari ya kuelekea kileleni.
Juanito
na wenzake wawili wameianza safari ya siku tano ya kupanda Mlima Kilimanjaro
kwa kutumia baiskeli wakipita lango la Kilema ambapo wanatarajia kupita katika
Kilele cha Mawenzi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea kilele cha Uhuru.
Mpanda
milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal(katikati) raia
wa Ureno na wenzake ,Ramon Abecia (kulia) na Eduardo Pascuaz wakiwa katika
picha ya pamoja na Mratibu wa safari hiyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni
ya Safari Bike Africa ,Mario Martos pamoja na waongoza watalii ,Ally Chuwa na
Elvas Mlengwa kabla ya kuanza safari ya siku tano kuelekea kilele cha Mlima
Kilimanjaro
Eduardo
Pascuaz akifunga kofia ngumu kabla ya safari ya kuelekea Kilele cha Uhuru
kuanza.
Mpanda
milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal(katikati) raia
wa Ureno na wenzake ,Ramon Abecia (kulia) na Eduardo Pascuaz wakijiandaa kuanza
safari ya siku tano kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro.