Mpanda milima
mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya
kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31
akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake
wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima
Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kupitia lango la Kilema.
Juanito
Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika
Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayo wakati wa
kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yamlima ambayo imekuwa ikibadilika kila
mara.