Hali ya simba mtoto aliyefanyiwa upasuaji mkubwa Novemba 9 ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kutokana na kuwa na tatizo la Ngiri, imeendelea kuimarika kwa kasi huku kundi la simba wa familia yake likimtenga na kuonyesha nia ya kumshambulia kwa kile kinachoelezewa na wataalam ni simba huyo mgonjwa kuonekana mgeni ndani ya familia yake baada ya upasuaji huo.
Kituo hiki kilifanikiwa kufika katika eno la Kreta ndani ya
hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia kazi kubwa ya uangalizi maalum anaopewa
simba huyo toka alipofanyiwa upasuaji wa tumbo hii ikihusisha kumtafutia
chakula na baadae kumrudisha katika kundi la simba wenzake kazi ambayo
inafanywa kwa umakini mkubwa.
(Kwa mujibu wa wataalamu hawa wanasema haikuwa kazi rahisi
kufanikisha mchakato mzima wa upasuaji wa simba huyo kutokana na uwezekano wa
kushambuliwa kwa simba huyo na wanyama wengine kama vile mbwa mwitu na fisi
ambao walionekana kumvizia usiku kucha kutokana na hali aliyokuwa nayo)
Kwa takribani siku nzima zoezi la kumuunganisha tena simba huyo
na familia yake linashindikana baada ya viashiria vya kushambuliwa kwa simba
huyo na sasa wataalamu wanachukua uamuzi wa kumhifadhi katika kibanda maalum
mpaka pale taratibu nyingine za kiuhifadhi na utawala zitakapo kamilika kutoka
mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.